Breaking

Tuesday, 30 May 2023

MTOTO WA MIAKA MIWILI AFARIKI KWA KUDONDOKEWA NA MAWE

Familia moja katika mtaa wa Eastleigh Jijini Nairobi sasa inatafuta haki baada ya jiwe kutoka jengo jirani lililokuwa linajengwa kumgonga na kumuua papo hapo. 


Mtoto mwenye umri wa miaka miwili alikuwa ndani ya nyumba ya wazazi wake wakati jiwe kubwa kutoka kwenye jengo lisilokamilika lilipasua paa la nyumba yao na kumuua papo hapo. 


Wazazi wake walimwambia Citizen TV kwamba mtoto huyo alikuwa kitandani wakati jiwe lilimuua siku ya Ijumaa, Mei 26. 


"Hili lilitokea saa moja usiku. Jiwe lilipasua paa letu na kumuua mtoto wetu. Tumefanya juhudi za kuwasiliana na mmiliki, lakini hatufikiwi. Tumetoa taarifa kwa polisi," alisema baba wa mtoto. 


Sehemu ya jengo linalojengwa iliporomoka. Vifusi vilivyokuwa vimeundwa na mawe ya ujenzi vilisababisha uharibifu mkubwa.

 

Mbali na kumuua mtoto, vilidondoka kwenye maduka jirani na kupasua paa. 


Wenyeji walisema hii sio mara ya kwanza mawe kutoka kwenye jengo hilo linalojengwa kusababisha hasara. 


Walisema kuwa hapo nyuma, vifusi vilidondoka na kuharibu magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu nalo na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. 


Via: Tuko News

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages