Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amefunga rasmi maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi jijini Arusha leo 22 Mei, 2023.
Akiwa kwenye ufungaji wa maonesho hayo amesema kuwa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanasaidia vijana kupata ujuzi wa kazi mbalimbali za kiufundi na kukuza ajira.
Amewataka washiriki kuendelea kutumia fursa hii hasa vijana kwa kuwa ni sehemu muhimu ya kujifunza na kupata uelewa katika sekta ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.