NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KITUO Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) imewataka Wananchi wanaoishi Jirani na maeneno ya hifadhi kuacha kuvamia katika maeneo yalianishwa kama hifadhi au mapori tengefu kwa mujibu wa sheria.
Wito huo umetolewa leo Mei 30,2023 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Anna Henga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu migogoro iliyopo kati TANAPA na wananchi wwaliopo katika maeneo ya hifadhi.
Dkt.Anna amesema wao kama taasisi ya haki za binadamu hawaungi mkono na wala hawana nia ya kuunga mkono wananchi kuvamia katika maeneo ya hifadhi yaliyoanishwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania
Aidha ameziomba mamlaka zinazohusika na uhifadhi ikiwemo TANAPA, TAWA na Wakala wa Misitu Tanzania(TFS) kuzingatia misingi ya haki za binadamu wakati wa utekelezaji wa amri za kuwaondoa na kuwahamisha wananchi katika maeneo ya hifadhi.