Na Humphrey Shao,
MKUU wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ,Mhe.Jokate Mwegelo ametoa onyo kwa wale ambao watahusika kwa namna moja ama nyingine kuhujumu miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa wilayani humo.
Jokate amesema hayo wakati wa uzinduzi wa programu Maalum ya kuhakikisha miradi yote iliyokwama inakamilika aliyoipa jina Operesheni Samia Maliza Miradi.
"Lengo letu ni kuona nambo mazuri ambayo Rais Dr.Samia Suluhu Hassan anayafanya kwa wananchi wake yanakwenda kama alivyo kusudia na ingekuwa tunategemea fedga za Mapato ya ndani peke yake tusingeweza kufanikisha hii miradi" amesema DC Jokate.
Amesema Serikali Kuu inazisaidia Serikali za mitaa kwa kuongeza fedha kwa kuwezesha miradi mbalimbali kikubwa wanachokifanya ni kusimamia fedha za Rais Dk.Samia kwa kuhakikisha thamani ya fedha ionekane na miradi ikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Aidha DC Jokate amesema ofisi yake haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa watumishi au mtu yoyote atakayehusika kukwamisha miradi hiyo.
Amesema moja ya vitu vya kujivunia kuwa Rais Samia suluhu Hassan ameweza kumletea fedha za Uviko 19 licha ya kujenga madarasa pia zimeweza kujenga jengo la huduma za dharura Wilayani korogwe.
Ametaja kuwa Korogwe ipo katika Barabara kubwa ya kuelekea mikoa ya Kaskazini hivyo uwepo wa jengo hilo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuhudumia watu ambao wamekuwa wakipata majanga katika njia hiyo.
Amesema huko nyuma ilikuwa mtu akipata dharura wanalazimika kuwapeleka watu maeneo ya mbali hivyo leo Mh Rais Samia ametusaidia kazi kwa kujengwa jengo hili .
"Kama viongozi kama wataalamu fedha zinaletwa ni mbegu tunapewa ni mbegu tunapewa, tuweke mikakati madhubuti fedha ile iliyoletwa iwe na tija Rais Samia kamaliza shughuli yake kazi imebaki kwetu sisi ,Viongozi wa Serikali,Viongozi wa chama na Watumishi wote pamoja na wananchi kwa ujumla, amesema DC Jokate.
Ametoa rai kwa wataalamu na watumishi wa Wilaya ya Korogwe kuhakikisha fedha zote zinazofika katika maeneo yao zinatumika sawasawa na maelekezo yaliyowajia.
Amesema kuwa ni haja sasa kuamua tukiwa kama Timu moja kufanya kazi kumaliza miradi yote na kwa thamani iliyotukuka.
Ameweka wazi kama viongozi lazima wakumbushane wizi na ubadhirifu wa fedha za umma katika Usimamizi wa miradi tuukatae ,ushirikiano kati ya Serikali na wananchi ni muhimu kwani ndio wenye hiyo , hivyo lzima tuwashirikishe na tuwape taharifa.
Pia amesema kuanzia Halmashauri, Tarafa, Kata mpaka kijiji zitoe taharifa ya fedha ambazo Serikali yao imewatengea.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo akishiriki kuchimba msingi wa nyumba za walimu shule ya msingi geza.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo akishiriki kujenga ukuta wa shule ya msingi geza Wilayani Korogwe
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo akishiriki kujenga zege la juu katika nyumba za walimu Korogwe.