NA EMMANUEL MBATILO MICHUZI TV
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said amesema kipindi cha Wazazi Super Cup ni kipindi cha kuingiza wanachama wapya na anategemea kupata tathmini ya wanachama wapya wa Jumuiya ya Wazazi baada ya Wazazi Super Cup.
Ameyasema hayo leo Mei 13,2023 wakati akifanya ziara katika Wilaya ya Ubungo na Kamati Tekelezi ambapo wamekutana na viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo.
Aidha Bi.Khadija amesema Kata ambazo wanaenda kucheza Wazazi Super Cup ametaka wenyeviti wa mtaa na madiwani washirikishwe kwani viongozi hao licha ya kuwa wanadhamana ya kiserikali wengine wamekuwa na uwezo hivyo ni rahisi kwenda kudumisha mahusiano kushirikiana na viongozi wetu.
Pamoja na hayo amesema kuwa Katika kipindi hiki ambacho tunakwenda kufanya Wazazi Super Cup wamezindua kampeni ya Ukatili wa Kijinsia ambapo wanaenda kuongelea na kupiga vita ukatili wa kijinsia lakini pia wanaenda kuongelea malezi chanya kwa wazazi na watoto wetu kwani wazazi ndo chanzo cha mambo mengi yanayoendelea sasa katika jamii yetu
"Sisi wazazi ndo tunakumbatia marafiki sio, sisi ndo tumeitambulisha kigodoro na kukaribisha mengine......turudishe mila na tamaduni na utambulisho wa Mtanzania tukiannza na sisi wazazi wenyewe kwanza tujue nini maana ya kuwa mzazi na nini maana yakuwa mlezi". Amesema Bi.Khadija
Kwa upande wake Katibu Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ubungo Bw.Gaus Kampendeza amesema Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ubungo imeweza kutatua migogoro inayojitokeza ndani ya chama kwa baadhi ya viongozi na kuleta suluhu pia wamekuwa wakitembea kwenye ofisi za kata kuhakikisha wanahamasisha maadili mema ili kulinda jamii yetu kupitiamilana tamaduni za Mtanzania
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mara baada ya kufanya ziara wilayani Ubungo leo Mei 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mara baada ya kufanya ziara wilayani Ubungo leo Mei 13,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said akikabidhi jezi kwa timu ambazo zinashiriki Wazazi Super Cup mara baada ya kufanya ziara wilayani Ubungo leo Mei 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ubungo Dkt.Meshaki Ole Sabaya akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said wilayani Ubungo leo Mei 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Katibu Elimu, Mlezi, Afya na Mazingira CCM Mkoa wa Dar es Salaam Laurian Mganga akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said wilayani Ubungo leo Mei 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa Baraza la Wazazi CCM Temeke Bw.Sharif Jumbe akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said wilayani Ubungo leo Mei 13,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said akisalimiana na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake wilayani Ubungo leo Mei 13,2023 Jijini Dar es SalaamMwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said akisalimiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo wakati wa ziara yake wilayani humo leo Mei 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Said wakati alipofanya ziara wilayani Ubungo leo Mei 13,2023 Jijini Dar es Salaam
(PICHA NA EMMANUEL MBATILO))