Breaking

Saturday, 27 May 2023

ASAKWA KWA TUHUMA ZA KUMTOBOA JICHO, KUMNG'OA JINO MPENZI WAKE




Isaack Mnyagi mkazi wa Sombetini jijini Arusha anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpiga mwenza wake, Jackline Mnkonyi (38) na kisha kumng’oa jino la mbele na kumtoboa jicho.


Tukio hilo limetokea juzi Alhamisi Mei 25, 2023 baada ya kutokea ugomvi ambao unadaiwa kuchangiwa na wivu wa mapenzi baina ya wenza hao.


Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni ,Daraja Mbili jijini Arusha, Jackline ambaye anamtoto mchanga amesema amepigwa na mumewe baada ya kumtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mgeni aliyefika nyumbani bila kujua Kama ni mjomba wake.


Amesema Mei 23, 2023 alitembelewa na Mjomba wake, Vicenti Matai kutoka mkoani Simiyu kwa lengo la kumsalimia baada ya kuondoka mgeni huyo mume wake saa 4.45 usiku alianza kumuhoji. 


Jackline amesema alimweleza Mgeni huyo alikuwa na mjomba wake lakini mumewe alikataa na ndipo alipoanza kumshambulia kwa ngumi, mateke na mkanda na baadaye alichukua Praizi na kumng'oa jino kwa nguvu.


"Nilijitahidi sana kujieleza lakini ilishindikana alianza kunipiga kwa mateke na ngumi na alichukua Praizi na kuniamuru nifungue mdomo na kuning’oa jino moja ambapo damu zilianza kuchuruzika,”amesimulia kwa uchungu huku akilia.


Amesema licha ya kipigo hicho pia alichukua kitu chenye ncha kali na kumtoboa jicho moja ambalo hadi sasa hawezi kuona huku akimwambia maneno mazito na kumtishia kumuua.


Amesema baada ya tukio hilo alimchukua na kumpeleka nyumbani kwa wazazi wake Sinoni Daraja mbili na kumtumpa getini.


Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Justin Masejo amesema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kumtafuta mtuhumiwa.


"Tunamtafuta aliyefanya uhalifu huu na akipatikana hatua za kisheria zitachukuliwa"amesema.


Via: Mwananchi


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages