Wizara ya Maliasili na Utalii imeibuka mshindi namba moja kwenye mbio za mita 800 kwenye mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea mkoani Morogoro.
Akizungumza leo mkoani humo mara baada ya ushindi Elibariki Buko ambaye ndio mshindi namba moja wa mbio za mita 800 kutoka Wizara hiyo, amesema ushindi huo utasaidia kuimarisha michezo na kuutangaza utalii Ili kuunga mkono juhudi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya 'The Royal Tour' za kutangaza utalii.
" Ushindi huu ni muhimu sana kwetu, tunaushukuru uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuhamasisha michezo. Ushindi huu ni moja ya sehemu ya kusaidia juhudi za kutangaza utalii kupitia filamu ya The Royal Tour ya Rais wetu mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. SAMIA Suluhu Hassan." alisema Buko.
Naye, Afisa Utalii Mkuu na mmoja kati ya Viongozi wa Timu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Martin Mrema amesema Wizara itahakikisha inaendelea kupambana ili kushinda michezo iliyobakia.
" Tumefurahi tumeshinda riadha, lakini si riadha tu, tumekuja kupambana na tutahakikisha tunatangaza utalii kupitia michezo. alisema.
Jumla ya michezo 10 imechezwa, kwa upande wa wanaume mbio za za mita 1500 Elibariki Buko alishika nafasi ya 02 ,huku mbio za mita 3000 Kispani Saigoti akishika nafasi ya 02 huku Athumani Simbiri akishika nafasi ya 03 katika mbio za mita 300 na 400.
Kwa Upande wa wanawake, mbio za mita 800 Jehovanesa Sarakikya alishika nafasi 03 na mbio za mita 1500 akishika nafasi ya 03.