Breaking

Sunday 16 April 2023

WATU 11 WAFARIKI AJALI YA BASI

Watu kumi na mmoja wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali eneo la Josa Area barabara ya Wundanyi-Mwatate Taita Taveta nchini Kenya.


Abiria wengine pia wamepata majera mabaya na kukimbizwa hospitalini juhudi za kuokoa maisha yao zikiwekwa. 


Basi hilo lilikuwa likitoka mazishi wakati ajali hiyo ilifanyika na likabingirika mara kadhaa watu wtano wakifariki papo hapo siku ya jumamosi.


Kamanda wa polisi eneo la Mwatate Morris Okul amedhibitisha ajali hiyo akisema shughuli za uokoaji zilianza mara tu ajali ilitokea. 


"Kwa sasa hatuwezi kujua kwa uhakika walioangamia kutokana na ajali hiyo," alisema Okul. 


Video iliyochapishwa mtandaoni ilionesha wasamaria wema wakijaribu kuokoa waliokuwa wamehusika katika eneo la mkasa. 


Katika ajali nyingine jijini, mtu mmoja alifariki dunia baada ya gari lao la kibinafsi kugonga trela iliyokuwa imeegeshwa kando ya baarabara. 


Mtu huyo alikuwa abiria kwenye gari hilo huku dereva naye akikimbizwa hospitalini.


Chanzo: Tuko news

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages