Breaking

Tuesday, 11 April 2023

WAMILIKI WA ARDHI NCHINI KUANZA KUPOKEA BILI ZA KODI YA ARDHI KUPITIA SIMU YA MKONONI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati Makamu wa Rais Dkt Philip Isdori Mpango aliposimama kwa muda kuzungumza na wananchi wa eneo la Hungumalwa wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakati wa mwanzo wa ziara yake ya siku tatu mkoani humo tarehe 11 April 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdori Mpango akuzungumza na wananchi wa Humgumalwa wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakati wa mwanzo wa ziara yake mkoani humo tarehe 11 April 2023.

Sehemu ya wananchi Hungumalwa wilayani Misumgwi mkaoni Mwanza wakifuatilia maelezo ya viongozi mbalimbali wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango tarehe 11 April 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipunga mkono wakati wa mwanzo wa ziara ya Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango mkoani Mwanza tarehe 11 April 2023.

Baadhi ya wana CCM wakiwa katika mapokezi ya Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango mkoani tarehe 11 April 2023.

………………………………

Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesema wamiliki wa ardhi nchini hivi karibu wataanza kupokea bili za kodi ya pango la ardhi kupitia simu ya mkononi

Dkt. Angelina Mabula ameyasema hayo leo tarehe 11 April 2023 wakati Makamu wa Rais Dkt philip Isdori Mpango aliposimama kwa muda kuzungumza na wananchi wa Hungumalwa wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakati wa mwanzo wa ziara yake ya siku tatu mkoani humo.

“Ninapozungumza sasa mikoa kumi tayari imeunganishwa katika mfumo na tutaanza kupata bili zetu kupitia simu ya mkononi hivi karibuni maana watu walikuwa wakihoji kama maji waliweza kwanini ardhi wasiweze”. Alisema Waziri Mabula.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa sasa kuna wataalamu 26 wanaboresha mifumo ndani ya wizara hiyo lengo likiwa kuhakikisha mifumo ya wizara inaimarika katika masuala ya malipo ili kuwawezesha miliki wa ardhi kuondokana na changamoto za ulipaji kodi ya pango la ardhi.

” Napenda niwahakikishie wanannchi wa Hungumalwa, Kwimba na wana Mwanza kwa ujumla kuwa zile kelele za ardhi zinaenda kuisha kwa sababu mama Samia ameiwezesha wizara” alisema Dkt Mabula.

Aidha, amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua nchi na kuhitaji kuwa na wawekezaji na kubainisha kuwa wawekezaji lazima wakute ardhi zipo na zimepangwa na kuwekwa kwa uwekezaji.

“Niwaombe katika kutenga maeneo ya uwekezaji lazima tuhakikishe yametambuliwa na yanamilikiwa lengo muwekezaji akija asianze kuvutana na wananchi, halmashauri na serikali ya kijiji husika iwe imefanya utaratibu wa kulitambua eneo na kumiliki” alisema Dkt Mabula.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages