Breaking

Tuesday, 11 April 2023

TRA WAPOKEA NA KUZINDUA BOTI MBILI ZA DORIA

Boti za doria ambazo zimekabidhiwa na kuzinduliwa katika kituo cha forodha cha TRA leo Aprili 11,2023 Jijini Dar es Salaam 
Kamishna Mkuu wa TRA, Bw.Alphayo Kidata akizungumza katika hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa boti za doria na kampuni ya Amikan Ventures katika kituo cha forodha cha TRA leo Jijini Dar es Salaam Jijini Dares Salaam
Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA Bw. Said Athumani akizungumza 
katika hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa boti za doria na kampuni ya Amikan Ventures katika kituo cha forodha cha TRA leo Jijini Dar es Salaam Jijini Dares Salaam


*****************


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) wamefanya makabidhiano ya boti za doria na kampuni ya Amikan Ventures katika kituo cha forodha cha TRA Jijini Dares Salaam ambapo boti mbili zimekabidhiwa na kuzinduliwa kwaajili ya kuanza kazi.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Aprili 11,2023 Jijini Dar es Salaam katika hafla hiyo, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw.Alphayo Kidata amesema boti hizo zitafanya kazi ya doria katika pwani ya Tanzania na maziwa kupambana na vitendo vya magendo ambavyo vinahatarisha mipango ya TRA katika kukusanya mapato ya nchi.

Amesema waingizaji wa bidhaa bandia na bidhaa za magendo wamekuwa wakitumia mwanya wa urefu wa mpaka wa pwani ya bahari ya hindi kwa kuingiza bidhaa bandia ikijumuisha dawa, vyakula, mavazi, viatu, vifaa vya elektroniki, na vinywaji vyenye pombe.

"Uingizaji wa bidhaa kama hizi zinaathiri vibaya uchumi wa nchi kupitia kukosa mapato, kukwamisha ukuaji wa viwanda vya ndani na biashara halali, na kuathiri afya na usalama wa watumiaji". Amesema Bw.Kidata.

Aidha amesema gharama za ununuzi ya boti hizo zilipitishwa wakati wa bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 ambapo Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ilitenga bajeti ya Tsh 2.5 Billioni kwa ajili ya ununuzi wa boti mpya za doria. Hivyo basi boti hizo mbili ambazo wamekabidhi wameona wazipeleke zikafanye kazi za doria kwa mikoa ya Dar es salaam na Kigoma ambapo kuna matukio mengi ya magendo.

Kwa upande wake Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA Bw. Said Athumani amesema boti hizo ambazo zimekabidhiwa ni sehemu ya bajeti ya Tsh. Billioni 2.5 iliyotengwa katika mwaka wa Fedha 2021/2022.

Amesema Mchakato wa Manunuzi katika bajeti hiyo umehusisha boti tatu za wazi na moia va kufungwa, ambapo Kampuni ya Amikan Ventures Limited ilishinda kandarasi ya kutengeneza boti tatu za wazi kwa thamani ya Tshs 1,589, 109,302.82 yaani kila boti thamani yake ni Tsh. 529,703, 100.94.

"Kamishna Mkuu, leo tutakuomba upokee na kuzindua boti 2 badala ya boti 3 kwani boti moja ilianguka wakati wa kushusha bandarini na kupata hitilafu kubwa. Mkandarasi ametakiwa kuleta boti nyingine mpya kwa gharama zake. Amepewa muda wa miezi 8 kuanzia mwezi wa Machi 2023 awe amekabidhi boti hiyo". Amesema Bw.Athumani.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages