Breaking

Wednesday, 12 April 2023

TEA YAINGIA MAKUBALIANO NA KAMPUNI YA SAYARI SAFI LIMITED KUSHIRIKIANA KATIKA UBORESHAJI WA MAZINGIRA YA UPATIKANAJI WA ELIMU BORA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Bahati Geuzye na Mkurugenzi wa Sayari Safi Limited, Bi.Rehema Mbalamwezi wakisaini makubaliano maalumu ya kushirikiana katika uboreshaji wa mazingira ya upatikanaji wa elimu bora nchini, hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Bahati Geuzye na Mkurugenzi wa Sayari Safi Limited, Bi.Rehema Mbalamwezi wakipongezana mara baada ya kuingia mkataba wa makubaliano maalumu ya kushirikiana katika uboreshaji wa mazingira ya upatikanaji wa elimu bora nchini , hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Bahati Geuzye na Mkurugenzi wa Sayari Safi Limited, Bi.Rehema Mbalamwezi wakionesha mkataba wa makubaliano maalumu ya kushirikiana katika uboreshaji wa mazingira ya upatikanaji wa elimu bora nchini, hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam,

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Bahati Geuzye akizungumza katika hafla ya Makubaliano kati ya TEA na Kampuni ya Sayari Safi Limited kushirikiana katika uboreshaji wa mazingira ya upatikanaji wa elimu bora nchini, hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Bahati Geuzye akisisitiza jambo wakati akizungumza
katika hafla ya Makubaliano kati ya TEA na Kampuni ya Sayari Safi Limited kushirikiana katika uboreshaji wa mazingira ya upatikanaji wa elimu bora nchini, hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sayari Safi Limited, Bi.Rehema Mbalamwezi akizungumza katika hafla ya Makubaliano kati ya TEA na Kampuni ya Sayari Safi Limited kushirikiana katika uboreshaji wa mazingira ya upatikanaji wa elimu bora nchini , hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Bahati Geuzye akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Kampuni ya Sayari Safi Limited pamoja na watumishi wa TEA katika hafla ya Makubaliano kati ya TEA na Kampuni ya Sayari Safi Limited kushirikiana katika uboreshaji wa mazingira ya upatikanaji wa elimu bora nchini, hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************


MAMLAKA ya Elimu Tanzania TEA imesaini makubalino maalumu ya kushirikiana katika uboreshaji wa mazingira ya upatikanaji wa elimu bora
na Kampuni ya Sayari Safi Limited ambayo inahusika na usambazaji wa maji safi na salama mashuleni ili kwa pamoja wafikishe huduma hiyo katika shule zote za Msingi na Sekondari hapa nchini.

Katika makubaliano hayo, awamu ya kwanza Kampuni ya Sayari Safi Limited imetenga kiasi cha Dola za Kimarekani Laki moja na nusu (Tsh.Milioni 351,304,350.00) ambayo moja kwa moja imeelekezwa kusaidia usambazaji wa maji mashuleni hapa nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo ambayo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye amesema, Mamlaka hiyo imekuwa na utaratibu wa kutekeleza miradi mbalimbali ya elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na mpaka sasa wameshafanikiwa kutekeleza miradi mingi.

Aidha ameipongeza kampuni hiyo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari ili kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa bora.

Amesema kupitia TEA, wamekuwa wakijenga madarasa, mabweni, matundu ya vyoo, ofisi za walimu kutoa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwenye shule mbalimbali za msingi, sekondari na vyuo mbalimbali.

Hata hivyo ameeleza kuwa Sayari Safi Limited wanahusika na kusambaza maji safi kwenye shule mbalimbali na kupitia makubaliano hayo watafanya kazi kwa ushirikiano ili kuzifikia shule nyingi zaidi za jijini Dar es Salam na za mikoa mbalimbali.

“Sayari safi watatoa huduma ya maji safi na salama mashuleni kwenye mikoa mbalimbali nchini lakini kwa kuanzia wameamua kuanzia jijini Dar es Salaam na kadri rasilimali zitakavyokuwa zinapatikana tutakauwa tukishirikiana kwenda kwenye shule za mikoa mingine ili wanafunzi wengi wapate majisafi na salama,” Amesema Bi.Geuzye.

Nae Mkurugenzi wa Sayari Safi Limited, Bi.Rehema Mbalamwezi, amesema kampuni hiyo inajikita katika miradi ya maji safi na salama kwenye shule za sekondari na msingi kwenye nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Msumbiji, Malawi na Zambia.

Amesema nia yao ni kuwawezesha wanafunzi na walimu kupata maji safi na salama ili kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko hali ambayo inaweza kuwapunguzia siku zao za kuwa shuleni na kwamba wataanza na shule 100 za jijini Dar es Salaam.

“Tutaendelea kuweka mifumo hii kwenye shule nyingi kwasababu tatizo la maji ni tatizo kubwa dunia nzima na asilimia 70 ya bajeti za afya kwnye nchi mbalimbali duniani inatumika kutibu magonjwa yanayotokana na kunywa maji yasiyo salama, kwa hiyo kwa mchango wetu wa kuhakikisha maji safi yanapatikana wanafunzi watasoma na kuwa shuleni muda mrefu,” Amesema

“Tatizo la majisafi na salama siyo la Tanzania tu ni la dunia nzima kwa sababu takribani watu bilioni 1.9 hawana uhakika wa maji safi na salama ya kunywa na watu bilioni 2 hawana vyoo kwa hiyo nasisi watanzania tuko kwenye hiyo changamoto ambayo inapaswa tukabiliane nayo,” ameeleza.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages