Na John Mapepele
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu, Dkt Hassan Abbasi leo amekutana na Menejimenti na watumishi wote wa Hifadhi ya Ngorongoro na kufanya kikao huku akiwataka kufanya kazi kwa kuzingatia weledi katika utekelezaji wa kazi za kila siku za kuhifadhi raslimali na kutangaza vivutio vya utalii duniani.
Mkutano huo pia umehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu ndugu Anderson Mutatembwa.
Aidha, amesema kila mmoja katika eneo lake lazima atekeleze majukumu yake huku akifafanua kuwa taasisi hii ni miongoni mwa taasisi ambazo zinatakiwa kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.
Amesema ili kufanya vizuri ni lazima pia kuzingatia misingi ya maadili, kuepukana na rushwa.
Katika hatua nyingine amewataka watendaji kufuatilia haki za watumishi hususan eneo la mvomeloupandaji wa madaraja kwa watumishi wenye sifa za kupandishwa vyeo.
Mara baada ya kufanya mkutano amekagua ujenzi wajengo ya ofisi ambapo amewataka kukamilisha ujenzi huo mapema kulingana na mkataba.
Pia ametoa wito kwa wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika maeneo ili Taifa liweze kuongeza mapato.