Breaking

Wednesday, 26 April 2023

HATUWEZI KUKAA KIMYA KATIKA KUZUNGUMZIA MMOMONYOKO WA MAADILI KWA VIJANA-VETA CHANG'OMBE

Chuo cha VETA Chang'ombe Dar es Salaam kimesema kuwa kutokana na mmomonyoko wa maadili nchini hawataweza kukaa kimya katika kuwaeleza vijana juu maadili hayo ikiwemo katika mapenzi ya jinsia moja.


Hayo ameyasema Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi Joseph Mwanda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na chuo kilivyojipanga katika ukemeaji kwa wanafunzi kutojihusisha na mmomoyoko wa maadili hayo.


Mwanda amesema Chuo kinazalisha ujuzi kwa vijana kwenda kutoa huduma mbalimbali ikiwemo viwanda hivyo haitakuwa na maana ya kuwa na vijana hao kwenye maeneo kuonyesha ujuzi wakiwa wasagaji au mashoga.


Aidha amesema katika kipindi cha hivi karibuni wamekutana na wanafunzi na kueleza hayo ikiwemo kuwa chuo hakikubaliani kuwepo makundi hayo na kuwataka vijana kujifunza ujuzi kutokana na serikali kuendelea kuwa na nchi ya viwanda huku Rais Samia Suluhu Hassan akiwa amefungua mipaka.


Mhandisi Mwanda amesema kuwa kuna uhitaji wa mafundi katika sekta ya viwanda hivyo mashoga na wasagaji hawana nafasi kwenye sekta hiyo.


"Utakuwaje na Fundi ambaye ni shoga wakati kuna kazi anatakiwa kutumia sehemu ya nguvu yake akiwa shoga hawezi kufanya hivyo na kufanya waandazi kuonekana hawakutimiza wajibu wao" amesema Mhandisi Mwanda.


Mratibu wa Dawati la Jinsia Chuo cha VETA Chang'ombe Hawa Nkunya amesema kuwa kuna mmomoyoko wa maadili hivyo kazi kubwa ni kupinga mmomoyoko huo na kufanya watu waliokuwa wanafikiria kufanya ushoga u usagaji kuacha.


Amesema kuwa kuna jitihada zinafanyika ikiwemo kuwa na mdahalo wa vijana kueleza madhara ya mmomonyoko wa maadili katika Taifa hususani katika sekta ya viwanda kukosa nguvu kazi ambayo sehemu kubwa ni vijana.


Amesema kuwa malezi ya vijana yako katika sehemu mbili ambazo ni Chuo na majumbani wanakotoka hivyo kunahitaji wazazi kushirikiana kuhakikisha mabadiliko hasi hayotokei kwa vijana na hao.


Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Temeke Devotha Nchia amesema kuwa kazi kubwa kwao ni kutoa elimu juu ya mmomonyoko wa maadili na madhara katika nyanja mbalimbali za kiuchumi.


Devotha amesema kuwa vijana wakiwa mashoga kama taifa litakosa nguvu kazi na idadi ya watu itapungua kutokana na wanaume kuacha kuzalisha na kuendelea kufanya mapenzi ya jinsia moja na wanawake kusagana ambapo pande zote hawezi kutokea mtoto.


Aidha amesema serikali imekuja na mikakati ya kuhakikisha kama Taifa tunafaata tamaduni zetu na sio kuiga tamaduni zingine.


Mwanafunzi Elizabeth Benard amesema kuwa kungekuwepo na sheria kwa wanaofanya na wanaofanyiwa kuwa na kifungo ambapo hiyo ndio itakuwa suluhu ya kutokomeza ushoga na usagaji.


Amesema kuwa vijana wana vitu vya kufanya na kujiletea maendeleo na sio kujiingiza katika ushoga na usagaji ambapo mwisho wa siku ni madhara kwao. .
Mkuu wa Chuo Ufundi Stadi VETA Chang'ombe Dar es SalaamMhandisi Bw.Joseph Mwanda akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi yake jana Aprili 25,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Dawati la Jinsia Chuo cha VETA Chang'ombe Bi.Hawa Nkunya akizungumza na waandishi wa habari jana Aprili 25,2023 VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Temeke Devotha Nchia akizungumza na waandishi wa habari jana Aprili 25,2023 VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA Chang'ombe Dar es Salaam wakipewa elimu kuhusu kupinga masuala ya ukiukwaji wa maadili
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages