**********
KAMISHINA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya DCEA), Aretas James Lyimo ametaja malengo yake ambayo ameingia nayo ili kuhakikisha mamlaka hiyo inadhibiti kabisa biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.
Ameyasema hayo leo Aprili Mosi, 2023 mkoani Mtwara wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambapo mamlaka hiyo inashiriki kikamilifu katika mbio za mwenge huku akiweka wazi mipango yake ya kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo.
"Kwa hiyo nitoe wito kwa watumiaji wa dawa za kulevya kuacha wenyewe kutumia dawa za kulevya, lakini pia kwa wale wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya kuacha kabisa hiyo biashara ya dawa za kulevya, kwani kuanzia sasa tunafanya operesheni kabambe nchi nzima, lakini tutahakikisha vijiwe vote vya wauzaji, na watumiaji wa dawa za kulevya tunavisambaratisha.
Mbio za Mwenge kitaifa kwa mwaka 2023 katika uwanja wa CCM Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara leo Aprili Mosi, 2023 zimezinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri va Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Aidha, Kamishana Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas James Lyimo amesema, ushiriki wao katika mbio hizo una umuhimu mkubwa.
"Tupo hapa Mtwara katika tukio hili la uwashaji wa Mwenge, kwa sababu Mwenge unatembea nchi nzima kwa ajili ya kukemea maovu, kuhakikisha kwamba, maovu yanaondoka kwenye jamii nchini, na sisi kama Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, dawa za kulevya ni sehemu moia wapo va maovu ambayo yanakemewa na Mwenge.