Breaking

Thursday, 27 April 2023

DAWASA YAFUNGUA DAWATI HUDUMA KWA WATEJA MAJOHE


 Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imefungua Dawati la huduma kwa wateja kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma juu ya huduma mbalimbali za Mamlaka ikiwemo utaratibu wa upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa Kata ya Majohe, Wilaya ya Ilala ambao ni sehemu ya wanufaika wa utekelezaji wa mradi wa maji Majohe.

Utekelezaji wa mradi wa maji Majohe umehusisha ulazaji wa mabomba ya inchi 8,6,4 na 3 kwa umbali wa kilomita 46 na utahudumia wananchi takriban 24,000.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages