Wananchi mbalimbali wamejitokeza na kutembelea banda la DAWASA katika tamasha ya kutangaza fursa za maendeleo na kupinga ukatili lenye kauli mbiu "zijue fursa kataa ukatili" ambapo mgeni rasmi ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt Dorothy Gwajima (Mb) linalofanyika katika viwanja vya leaders club Jijini Dar es Salaam.
DAWASA inawakaribisha wananchi kutembelea banda la maonyesho ili kufahamu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mamlaka katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora za Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam na Pwani.