Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba, Mwenyekiti wa Bodi DART Dkt. Florens Turuka,Mkurugenzi wa DART, Dkt. Edwin Mhede pamoja na viongozi wa NMB wakiwa katika uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba akipanda mche wa mti katika kando ya barabara ya mabasi yaendayo kasi wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023
Mwenyekiti wa Bodi DART Dkt. Florens Turuka akipanda mche wa mti katika kando ya barabara ya mabasi yaendayo kasi wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023
Mkurugenzi wa DART, Dkt. Edwin Mhede akipanda mche wa mti katika kando ya barabara ya mabasi yaendayo kasi wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba akizungumza wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023
Mwenyekiti wa Bodi DART Dkt. Florens Turuka akizungumza wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023.
Mkurugenzi wa DART, Dkt. Edwin Mhede akizungumza wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023
************
WAKALA wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), imepanga kupanda miti zaidi ya 1,000 kwenye kilomita 154 ambayo miundombinu ya mabasi yake inapita jijini hapa.
Hayo yalisemwa leo Aprili 12,2023 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa DART, Dkt. Edwin Mhede, wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti hiyo kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam wamiwemo wa benki ya NMB.
Dk. Mhede alisema kabla ya ujenzi wa miundombinu ya mwendokasi kulikuwa na uoto wa asili na miti ya aina mbalimbali hivyo DART inawajibika kuirejesha hali ilivyokuwa.
“Sisi tunapojenga barabara kwa kiasi kikubwa tunaharibu uoto wa asili na miti kwasababu kama kulikuwa na mti tunaukata na nyinyi mliokuwa Dar es Salaam wakati huo naamini mnakumbuka hali ilivyokuwa hapa Ubungo kabla ya ujenzi huu, ile hali haipo tena ndiyo sababu tunaona tunawajibika kuirejesha,” alisema Dk. Mhede
Alisema asilimia 45 ya wakazi wa Dar es Salaam wanatumia njia za kwenda kwa miguu (shoroba), ambazo kwa sasa hazina miti ambayo zamani iliwasaidia kupita kivulini hali ambayo alisema lazima irejelezwe.
“Nitoe wito kwa watumiaji wa hizi njia za kwenda kwa miguu waitunze hii miti kwasababu itakuwa msaada mkubwa kwao tumeanza kupanda miti leo lakini tutaendelea mpaka kufikia miti zaidi ya 1,000,” alisema
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba, alisema uzinduzi wa upandaji miti hiyo ni jambo kubwa na la kihistoria kwa wakazi wa Ubungo na jijini Dar es Salaam kwani itasaidia kwa kiwango kikubwa kurejeleza mazingira yaliyoharibiwa kutokana na shughuli mbalimbali za ujenzi.
“Mazingira ni uhai hivyo ukiyahifadhi mazingira na yenyewe yatakuhifadhi ukiyaharibu na yenyewe yatakuadhibu kwa hiyo natoa wito kwa wananchi wa Ubungo waunge mkono kampeni hii kwa kutunza miti itakayopandwa, kila mtu ambaye miti hii itapandwa mbele ya nyumba yake au eneo lake la biashara atawajibika kuitunza” alisema
Mkuu huyo wa Wilaya alisema alishatoa maelekezo kwa viongozi wa mitaa na kata kuitambua miti hiyo na kuitunza kwa hali na mali itakapopandwa na DART na wafanyabiashara ndogo ndogo wafanye biashara zao sehemu ambazo hazina miti.
“Wafanyabiashara ndogo ndogo lazima wajue umuhimu wa kutunza mazingira kwaajili yao na vizazi vijavyo na wakumbuke kwamba ukiyalinda mazingira na yenyewe yatakulinda kwa hiyo kila mmoja wetu awe mlinzi wa mazingira kwa kuhakikisha miti hii inastawi,” alisema
Aliwataka watanzania kuona fahari ya kupanda miti kwa kushiriki vyema kwenye kampeni ya upandaji miti kwa Mkoa mzima akisema kuwa hata yeye binafsi amekabidhiwa mti ambao ameupanda na kuuwekea alama kwaajili ya kuhakikisha anafuatilia ukuaji wake.
“Huu mti ambao nimeupanda leo nimeagiza wauwekee alama ili niwe naupitia mara kwa mara kuumwagilia na kuuwekea mbolea na mti huu utakapokuwa nitakuwa nimetoa mchango mkubwa kwa taifa katika kuhifadhi mazingira,” alisema
Alisema viongozi wa kitaifa, Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha upandaji wa miti kwaajili ya kuhifadhi mazingira hivyo wananchi wanapaswa kuiga mfano huo na kupanda miti.