Breaking

Friday, 31 March 2023

WOMEN FOR CHANGE WATOA MSAADA WA MASHINE ZA KUSAIDIA KUPUMUA WATOTO NJITI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SHINYANGA

Wakikundi cha Women For Change wakipiga picha ya kumbukumbu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga walipofika kukabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) 
Viongozi wa Kikundi cha Women For Change (kushoto) wakikabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) ambao mapafu hayajakomaa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mashine za kusaidia watoto kupumua zikiwa kwenye maboksi
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC), kinachojihusisha na Ununuzi wa Hisa ili kuinuana kiuchumi na chenye mfuko wa kusaidia jamii na watoto walioko kwenye mazingira magumu kimetoa msaada wa mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) ambao mapafu hayajakomaa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Women For Change wamekabidhi mashine ‘cPAP’ mbili zenye thamani ya shilingi Milioni 2.4 kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila leo Ijumaa Machi 31,2023 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike

Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo, Mwenyekiti Msaidizi wa Kikundi cha Women For Change, Lucy Mwita amesema mashine hizo zitasaidia kupumua kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda ambao mapafu yao hayajakomaa.

Kikundi chetu cha Women For Change, kina wanachama 20, tunajihusisha na Ununuzi wa Hisa ili kuinuana kiuchumi na tuna mfuko wa kusaidia jamii na watoto walioko kwenye mazingira magumu.

Tumekuwa tukisaidia katika sekta ya elimu kwa kuchangia madawati,kukarabati mabweni na shughuli mbalimbali, leo tumekuja kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya afya kwa kuchangia mashine hizi (cPAP) zenye thamani ya shilingi milioni 2.4 ili kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (njiti)”,amesema Lucy ambaye ni Mkurugenzi wa Shule za Little Treasures.

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yustina Tizeba amesema hospitali hiyo imekuwa ikipata watoto wengi wanaozaliwa kabla ya muda ‘Pre –mature’ hivyo mashine hizo zitasaidia sana kuokoa maisha ya watoto.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila amekishukuru Kikundi cha wanawake ‘Women For Change’ kwa msaada huo kwani watoto wanaozaliwa kabla ya muda wanapata shida katika upumuaji hivyo wameokoa maisha ya watoto.
Mwenyekiti Msaidizi wa Kikundi cha Women For Change, Lucy Mwita akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ambapo wamekabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti Msaidizi wa Kikundi cha Women For Change, Lucy Mwita akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ambapo wamekabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mwanachama wa Kikundi cha Women For Change, MC Mama Sabuni akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ambapo wamekabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Women For Change, Ansila Benedict maarufu Lulekia akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ambapo wamekabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Women For Change,  Ansila Benedict akikabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Aliyevaa tai katikati ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila.
Viongozi wa Kikundi cha Women For Change (kushoto) wakikabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Aliyevaa tai katikati ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila akizungumza wakati Kikundi cha Women For Change kikikabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yustina Tizeba akizungumza wakati Kikundi cha Women For Change kikikabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wakikundi cha Women For Change wakipiga picha ya kumbukumbu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga walipofika kukabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) 
Wakikundi cha Women For Change wakipiga picha ya kumbukumbu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga walipofika kukabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) 
Wakikundi cha Women For Change wakipiga picha ya kumbukumbu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga walipofika kukabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) 
Wakikundi cha Women For Change wakicheza muziki katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga walipofika kukabidhi mashine za kusaidia kupumua kwa watoto (njiti) 

Watumishi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

 Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages