Breaking

Friday, 17 March 2023

TMDA YATOA ELIMU YA MATUMIZI  SAHIHI YA DAWA KWA SHULE ZA SEKONDARI KINONDONI

Mkaguzi Msaidizi-TMDA Bw.Boniphace Likati akizungumza na wanafunzi katika programu ya utoaji elimu kuhusu Matumizi sahihi ya Dawa na Vifaa Tiba kwa wanafunzi wa shule za Sekondari Wilaya ya Kinondoni leo Machi 17,2023 Jijini Dar es Salaam.

***********

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) imeweza kutoa elimu ya matumzi ya dawa na vifaa tiba katika shule 32 za Sekondari wilayani Kinondoni, ambapo walimu na wanafunzi 24,744 wameweza kupatiwa elimu hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Machi 17,2023 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Kanda ya Mashariki-TMDA, Bw. Adonis Bitegeko amesema katika mwezi Machi mwaka huu wameutumia katika kutoa elimu kwa wnaafunzi kwani ni kundi kubwa katika jamii ambalo likielimishwa litaweza kuifikia jamii kwa ukubwa zaidi na hasa kaya ambazo wanafunzi hao wanaishi.

Aidha amewataka wananchi kwamba endapo watakuwa wamepata madhara kutokana na matumizi ya dawa au vifaa tiba basi watoe taarifa TMDA kwa kupitia namba yao ya simu ya kupiga ya bure 0800110084.

Pamoja na hayo Bw.Bitegeko ameushukuru uongozi wa Manispaa ya Kinondoni hasa Idara ya Elimu kuwawesesha TMDA kutoa elimu katika Wilaya hiyo, pia amewashukuru walimu pamoja na wanafunzi kutoa ushirikiano mkubwa katika kipindi hicho.

Nae Mwakilishi wa Afisa Elimu, Shule za Sekondari Wilaya ya Kinondoni, Mwl.Cleopa Soi amesema programu ambayo wameianzisha TMDA katika utoaji elimu ya matumizi sahihi ya Dawa na Vifaa Tiba katika shule hizo imeweza kuwagusa walimu na wanafunzi wengi kwani wamepeleka ujumbe muhimu na adhimu.

"Naishukuru na kuipongeza TMDA kwa kutoa wito kuanzishwa kwa vilabu katika shule zetu na kuwaalika wanafunzi kuweza kutembelea, ni jambo jema na linamanufaa katika jamii na taifa kwa ujumla". Amesema Mwl. Soi.

Kwa upande wa Wanafunzi wameishukuru kupata elimu hiyo kwani imewajengea uelewa mkubwa katika matumizi sahihi ya dawa ambazo wanatumia pindi wanapokuwa wagonjwa.

"Jamii imekuwa na fikra duni kuhusiana na masuala ya dawa hivyo kupitia elimu tuliyoipata kutoka TMDA tutahakikisha tunapeleka elimu hii kwenye jamii ili na wengine waweze kuelewa matumizi sahihi ya dawa". Amesema Aisha Kondo mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Makumbusho.

Mkaguzi Msaidizi-TMDA Bw.Boniphace Likati akizungumza na wanafunzi katika programu ya utoaji elimu kuhusu Matumizi sahihi ya Dawa na Vifaa Tiba kwa wanafunzi wa shule za Sekondari Wilaya ya Kinondoni leo Machi 17,2023 Jijini Dar es Salaam.Meneja wa Kanda ya Mashariki-TMDA, Bw. Adonis Bitegeko akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 17,2023 katika program ya utoaji elimu ya Matumizi sahihi ya Dawa na Vifaa Tiba kwa wanafunzi wa shule za Sekondari Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Programu hiyoo imeendeshwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Makumbusho, Mwl.Jackson Mulinda akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 17,2023 katika program ya utoaji elimu ya Matumizi sahihi ya Dawa na Vifaa Tiba kwa wanafunzi wa shule za Sekondari Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Programu hiyoo imeendeshwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Mwakilishi wa Afisa Elimu, Shule za Sekondari Wilaya ya Kinondoni, Mwl.Cleopa Soi akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 17,2023 katika program ya utoaji elimu ya Matumizi sahihi ya Dawa na Vifaa Tiba kwa wanafunzi wa shule za Sekondari Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Programu hiyoo imeendeshwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Makumbusho Aisha Kondo akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 17,2023 katika program ya utoaji elimu ya Matumizi sahihi ya Dawa na Vifaa Tiba kwa wanafunzi wa shule za Sekondari Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Programu hiyoo imeendeshwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Makumbusho Rajab Mkemwa akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 17,2023 katika program ya utoaji elimu ya Matumizi sahihi ya Dawa na Vifaa Tiba kwa wanafunzi wa shule za Sekondari Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Programu hiyoo imeendeshwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA)

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages