Breaking

Wednesday, 22 March 2023

MADEREVA BODABODA WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUPINGA VITENDO VYA UKATILI KWA WANAWAKE NA WATOTO


MADEREVA wa Bodaboda, wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kupinga na kukomesha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto, ili kunusuru taifa la kesho dhidi ya vitendo hivyo.

Kauli hiyo imetolewa Machi 20,2023 na Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni, wakati wa kufungua Mafunzo kwa Viongozi wa madereva bodaboda ndani ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Dkt. Nyoni amesema wanahitaji kuhakikisha vitendo vya ukatili vinaisha, kwani mtoto anaweza kafanyiwa ukatili akiwa mdogo ambapo huharibu uhusiana wake na maisha wakati wa ukubwani.

"Ukatili unamadhara ya kisaikolojia, na inaonekana kidonda kinapona lakini yale madhara yakisaikolojia huwa hayaponi, hasa kama ikikosekana huduma stahiki kwa wakati". Amesema Dkt.Nyoni.

Kwa upande wake Mratibu wa Kitengo cha Ushiriki Jamii na Mafunzo Bw.Dastan Haule, amesema wamelenga kukutana na makundi ya viongozi wa waendesha bodaboda kwa kuwajengea uwezo ili wao waweze kuongea na wenzao.

Naye, mmoja wa waendesha Bodaboda aliyeshiriki katika mafunzo hayo Bw.Musa Julius ameipongeza taasisi ya Ustawi wa jamii kwa mafunzo aliyoyaita mazuri na ameahidi kuwafundisha wenzake kuhusu ukatili wa kijinsi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages