Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Jokate Mwegelo amezuru nchini Afrika kusini wiki hii kutangaza umuhimu wa Vijana wa Afrika kushiriki katika Ujenzi wa Afrika.
Lengo kuu la ziara hiyo ni kutangaza zao la Mkonge na bidhaa zinazotokana na Mkonge, Masuala ya uhifadhi wa wanyamapori na Mazingira pamoja na Fursa za mazao Mengine yanayolimwa Wilayani Korogwe Mkoani Tanga. Hata hivyo atatumia fursa hiyo kutangaza Chapa ya ‘MADE IN KOROGWE’ ikiwa ni sehemu ya kutangaza bidhaa zinazalishwa Wilayani Korogwe Mkoani Tanga
Katika Ziara hiyo, Jokate atapata fursa ya kutangaza shughuli Mbalimbali zinazofanywa na wajasiriamali Wanawake na Vijana wa Kitanzania.
“Nina Furaha kutembelea Afrika kusini na kuungana na wafanyabiashara wengine na Viongozi ambao wanashiriki maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga Bara Bora la Afrika. Natarajia kushiriki Uzoefu wangu na Kujifunza Kwa wengine,” Jokate Mwegelo
Pia watajadili jinsi wajasiriamali wa Afrika kusini na Tanzania wanaweza kufanyakazi pamoja ili kukuza ukuaji na Maendeleo katika Bara la Afrika.
“Kuna Watanzania wengi sana Nchini Afrika kusini na Waafrika kusini ambao wanataka kuwekeza katika Nchi yetu hii imekuwa fursa nzuri sana ya Kujadili njia za ushirikiano,” Jokate Mwegelo.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo amesema Kuna fursa nyingi sana Korogwe kutoka katika bidhaa rafiki Kwa mazingira zinazotengemezwa na Wanawake wa Korogwe mkoani Tanga.