Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Charles Martin Hilary kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali. Charles Hilary ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano - Ikulu, Zanzibar.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena Said ameeleza kuwa uteuzi huo unaanza leo Jumatatu Februari 06, 2023