Breaking

Tuesday, 21 February 2023

OCD KILOMBERO ASIMAMISHWA KAZI



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni amemsimamisha kazi Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilombero (OCD) Shedracck Kigobanya huku akimuhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Upelelezi Wilaya hiyo (OC CID), Daud Mshana kwa kushindwa kuwasimamia Askari wake na kudaiwa kunyanyasa Wananchi na kuwabambikia kesi.

Maamuzi ya Waziri Masauni yamekuja baada ya Wananchi wa Mji wa Ifakara kulalamika katika mkutano wa hadhara kuwa kuna baadhi ya Askari Polisi wa Wilaya hiyo ya Kilombero wanatumia nafasi zao vibaya na kunyanyasa Wananchi.

Wananchi hao wanasema mara nyingi wawanapokamatwa hufikishwa katika Kituo cha Polisi Ifakara lakini lugha wanazopewa sio za kiuungwana huku wengine wakiwatuhumu kushirikiana na Watu wenye fedha na kuwapokonya haki Wananchi wanyonge.

Baada ya malalakimo hayo Masauni akatoa msimamo wa Serikali ambapo ameswasimamisha kazi na kuwahamisha Maofisa hao ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazotolewa za Wananchi kwa Jeshi la Polisi.

Masauni amenukuliwa akisema “Hivi karibuni tumewahamisha Askari Polisi wengi katika Mkoa huu akiwemo aliyekuwa RPC, Fortunatus Musilimu na sasa tumemleta Kamanda mwingine Alex Mkama hivyo sitarajii turudi tulikotoka niseme tu kwamba Askari mmoja akichafua Jeshi tutamshughulikia kama Mhalifu ili asiharibu taswira ya Jeshi letu"


Via: Millard Ayo
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages