Breaking

Friday, 3 February 2023

MAHAKAMA KANDA YA TABORA YAENDESHA MASHAURI 1,579 KWA MTANDAO



Na Lucas Raphael,Tabora

Mahakama kuu kanda ya Tabora imefanikiwa kuendesha mashauri 1,579 kwa njia ya mtandao ‘Video Conference’ na kusajili mashauri 4,254 na kuyatolea maamuzi 4,170 na hivyo kupunguza gharama na muda zaidi wa uendeshaji na kuleta tija kubwa kwa wahusika na Mahakama kwa mwaka 2022.

Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora Amour Hamisi wakati wa akizungumza na mwandishi wa habari hizi na kusisistiza kwamba mahakama imekuwa ikifanya maswala ya usuluhishi ili kuokoa gharama,muda na mlundikano wa mashauri Mahakamani.

Alisema kuwa utaratibu wa kutumia mitandao kuendesha mashauri ni mzuri kwa kuwa unaokoa muda,gharama na unaondoa malalamiko kuhusu rushwa,unakuwa wa uwazi zaidi ambapo dira ya Mahakama ni kusogeza huduma bora yenye weledi kwa jamii kwa kuzingatia haki na sheria.

Jaji huyo wa mahakama kanda ya tabora alisisitiza kwamba Uendeshaji wa mashauri kwa njia ya mtandao ‘Video Comference’ kumechochea Mahakama kupata mafanikio makubwa katika kufanya shughuli zake kwa weledi,uwazi,haraka,umakini,kuondoa madai ya rushwa,kupunguza gharama na muda.

“Mafanikioa ya usuluhishi yana athali chanya na yanapendwa na wahusika kwa kuwa wanakuwa huru zaidi kuliko Mahakamani.kazi ya msuhishi sio kutoa hukumu ni kusimamia malidhiano na kupatanisha”alsema.




Aliwataka watumishi wa MahakamA kuendeleza juhudi za kuwahumia jamIi kwa kutoa huduma bora kwa kuzingatia haki,weledi ,busara ,uadilifu wakimtanguliza Mungu pasipo kumuonea mtu ama kupindisha sheria.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya wanawake ya Shirikisho la vyama vya wafanyakazi TUCTA Taifa Rehema Ludanga akiongea na mwandishi wa habari hizi alisema kuwa wanajikita kutoa elimu na usuluhishi kwa waajiliwa na waajili kutambua na kujua haki,wajibu na kuelekeza mipaka yao kuondoa misuguanao isiyokuwa na lazima miongoni mwao.

Alisema kuwa mara kadhaa kumekuwapo na kutotendea haki kwa waajili na waajiliwa kutokana na kutofahamu mipaka, taratibu,kanuni na sheria hivyo kupelekea kutoa adhabu pasipo haki ama kupita kiwango na hivyo kuleta malumbano na manung’uniko.



“Kamati ya wanawake TUCTA ina wajibu wa kusimamia waajiliwa na waajili kutambua wajibu,haki,taratibu,kanuni na miongozo iliyopo pamoja na kila upande kujua mipaka yake ili kuondokana na kutotendea haki na kuumizana ama kukandamizana,tunafanya usuluhishi wenye tija kwa pande zote”alisistiza.

Ludanga alisema kuwa wataendelea kushirikiana na waajili na waajiliwa katika sekta mbalimbali nchini kuhakiksha kila upande unatambua na kutimiza wajibu wake ili kupunguza na kuhakikisha misuguano makazini inaondoka na kusimamia haki ipatikane pande zote kwa mujibu wa sheria.

MWISHO.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages