Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camillus Wambura, amefanya kikao na wakuu wa Polisi wa Usalama barabarani wa Mikoa yote Tanzania, wakaguzi wa magari na watahini wa madereva leo tarehe 21.02.2023 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa Kikao hicho kimelenga kuwakumbusha mambo ya kuzingatia katika utendaji kazi, usimamizi, ufuatiliaji na kuona namna bora ya kuondokana na ajali za barabarani ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa utoaji wa leseni za udereva.
Hii ni sambamba na kutoa mafunzo kwa wakaguzi wa magari na watahini wa madereva wapya ambao watapewa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatiE nidhamu, haki, weledi na uadilifu.
Akiongea na waandishi wa wahabari katika kikao cha ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camillus Wambura amesema "Jeshi la Polisi limefanya uchunguzi na kuona umuhimu wa kurekebisha mfumo wa utoaji wa leseni za udereva ili kudhibiti ajali za barabarani"