Breaking

Thursday, 2 February 2023

DKT. BITEKO AWATAKA WANACHAMA KUTANGAZA MAFANIKIO UTEKELEZAJI ILANI MIAKA 46 YA CCM




Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt. Doto Biteko amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kufanya Siasa za Utulivu na kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Biteko amebainisha hayo katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Geita ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Bukombe.

Aidha, Dkt. Biteko ameshiriki ujenzi wa Ofisi za CCM katika kata ya Bulangwa na Ofisi ya CCM ya tawi Kelezia kata ya Igulwa baada ya kuungana na wanachama wa CCM mkoa wa Geita kutembelea miradi minne (4) inayotekelezwa wilayani Bukombe ikiwemo miradi miwili ya maji na miradi miwili ya majengo ya Ofisi za CCM.

Pia, Dkt. Biteko ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Bukombe kutunza miradi yote ambayo Serikali kupitia Ilani ya CCM imewaletea katika wilaya hiyo na kuwataka wananchi wote kuwa walinzi wa miradi hiyo na kutunza miundombinu yake.

Naye, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicolaus Kasendamila amewataka viongozi wa CCM mkoa wa Geita kuwashirikisha Wahandisi wa Serikali katika mikoa na wilaya pindi wanapotekeleza miradi ya chama hicho.

"Niwaombe viongozi wa chama waodokane na mazoea ya kutekeleza miradi ya chama bila kushirikisha wahandithi ili majengo yasijengwe chini ya kiwango wakati wahandisi wapo," amesema Kasendamila.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM kata ya Bulangwa Edimund Majelezi amesema ujenzi wa ofisi ya CCM kata utagarimu sh 40 milioni lakini hadi sasa wananchama wamechagia sh 400,000 na wanatarajia kupata fedha za uendelezaji wa mradi huo toka kwa wadau.

Pamoja na mambo mengine, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella amewapongeza wabunge wote wa mkoa wa Geita kwa kutekeleza kwa vitendo ilani ya CCM ambapo amesema mkoa wa Geita umeletewa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya maji, elimu, afya na miundombinu ya barabara.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages