Breaking

Wednesday, 22 February 2023

DC MBINGA ATOA MAELEKEZO KWA WATENDAJI WA KATA, MAAFISA LISHE




Mkuu wa Wilaya ya Mbinga amewataka watendaji wa kata na maafisa lishe kushirikiana kuanzisha klabu za lishe katika shule mbalimbali hali itakayosaidia kuhamasisha la lishe bora.

DC Aziza ametoa maelekezo hayo wakati akiongoza kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe kwa robo ya pili ya mwaka 2022 kilichofanyika Februari 22, 2023.

Katika kikao hicho amepokea taarifa ya tathmini ya mkataba wa lishe kutoka kwa Maafisa lishe kutoka halmashauri ya wilaya ya Mbinga na halmashauri ya mji Mbinga.

Akiwasilisha taarifa ya tathmini ya mkataba wa lishe, Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya Ndugu Judith Mushi alieleza kwamba utekelezaji wa bajeti ya Lishe ya Lishe ilyopangwa oktoba hadi disemba imetumika yote kwa asilimia 100%, Vilevile utekelezaji wa shughuli za lishe uliofanyika kwa asilimia 100% ikiwa pamoja na elimu ya ulishaji watoto na upimaji madini joto pamoja na mafanikio ikiwa kata 24 kati ya 29 zilifanya siku ya Lishe katika maeneo yao.

Vilevile, Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mji Mbinga Ndugu Sheila alifafanua kwamba utekelezaji wa shughuli za lishe ulifanyika kwa ufanisi mkubwa na utekelezaji wa agizo la uboreshaji wa vyoo vya ofisi za Kata na Vijiji kutokuwa na vyoo vya kisasa unaendelea ambapo vingine vimekamilika na vingine vipo katika hatua za mwisho kukamilika.

Dc Aziza aliwataka watendaji kata wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga katika kata ambazo hazijafanya siku ya Lishe zifanye siku ya leo, Vilevile aliwataka watendaji wa kata kuendelea kujenga vyoo vya kisasa katika maeneo yao ambapo masink ya kukamilisha vyoo hivyo atatoa ili suala la lishe liende sambamba na mazingira Safi.

Amewataka Maafisa lishe wa Halmashauri zote mbili wahakikishe kila aina ya chumvi inayoingia ni lazima zipimwe ili kubaini kama zina madini joto yanayostahili kutumiwa na jamii, Vilevile alisisitiza kwamba chumvi zote zitakazokutwa hazina madini joto zinapaswa kuteketezwa kwa mujibu wa sheria ndogo za Halmashauri.

Vilevile aliwataka watendaji wa kata kuendelea kujenga vyoo vya kisasa katika maeneo yao ambapo masink ya kukamilisha vyoo hivyo atatoa ili suala la lishe liende sambamba na mazingira Safi.

Alikadhalika, aliwataka Maafisa lishe wa Halmashauri zote mbili wahakikishe kila aina ya chumvi inayoingia ni lazima zipimwe ili kubaini kama zina madini joto yanayostahili kutumiwa na jamii, Vilevile alisisitiza kwamba chumvi zote zitakazokutwa hazina madini joto zinapaswa kuteketezwa kwa mujibu wa sheria ndogo za Halmashauri.

Hata hivyo, Aliwataka watendaji wa kata na maafisa lishe kushirikiana kuanzisha klabu za lishe katika shule mbalimbali pamoja na kuhamasisha utunzi wa nyimbo ambazo zitahamasisha ujumbe wa lishe kama ilivyo katika sekta zingine za utalii na mazingira, kwa kufanya hivyo jamii itazoea na itakuwa rahisi kuzingatia na kumbukumbuka lishe.

Awali Mkuu wa Wilaya Mbinga aligawa masink saba ya vyoo kwa watendaji wa kata ambapo kata ya Mpepai aliwapa masink matatu (3), Kihungu masink 2 na kagugu masink mawili (2)

Aidha, alisisitiza anaendelea kuratibu mpango wa shule ambazo hazina huduma ya maji kabisa kupata huduma hiyo, ambapo shule ya msingi Tulila iliyopo kata ya Mpepai na shule ya msingi pacha sita iliyopo kata ya kihungu zitapata mradi wa Maji ya visima kwa awamu ya kwanza, ambapo alisema ataendelea kuratibu ili shule zote ambazo hazijafikiwa na mradi wa maji zipate.

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbinga OCD Majaliwa alisisitiza kwamba Maafisa lishe na watendaji wa kata kushirikiana na dawati la jinsi lililopo katika kila kata kutoa elimu Kwa wazazi ili hata pale migogoro ya kifamilia inapotokea wazazi wakatengana iwe rahisi kila mzazi kukumbuka wajibu wake kwa kuhakikisha watoto wanapata lishe bora.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages