Breaking

Friday 10 February 2023

BILIONI 16.5 ZATENGWA KUKARABATI HOSPITALI KONGWE



OR - TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange(Mb) amesema Serikali imetenga fedha shilingi bilioni 16.5 kufanya ukarabati wa hospitali 19 katika mwaka wa fedha 2022/23.

Amesema hayo leo tarehe 10 Februari 2023 Bungeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge Viti Maalum, Mhe. Esther Midimi aliyetaka kujua Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kwa kuwa Hospitali iliyopo ina hadhi ya Kituo cha Afya na haikidhi mahitaji.

Dkt. Dugange amesema Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ni miongoni mwa hospitali kongwe 50, ilianza kutoa huduma kwa ngazi ya Kituo cha Afya ambapo mwaka 1989 ilipandishwa hadhi na kuwa hospitali.

Aidha, Dkt. Dugange amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali itatenga fedha za ukarabati wa hospitali 31 zilizobakia ikiwemo hospitali ya Wilaya ya Meatu.

Dkt. Dugange amesema Serikali imeshafanya tathmini ya hospitali chakavu zote nchini na itaanza kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa hospitali hizo katika mwaka wa fedha ujao.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages