Watoto watatu wa familia moja wilayani Rorya mkoani Mara, wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Shirati wakipatiwa matibabu kwenye majeraha mbalimbali ya moto waliyochomwa na mwanamke anayedaiwa kuwa ni bibi yao aitwaye Eliza Odira (68).
Taarifa zimeeleza kuwa bibi huyo amemuoa kimila mama wa watoto hao (Nyumba ntobhu)ili amzalie watoto na kwamba chanzo cha ukatili huo bado hakijajulikana na bibi huyo yupo kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.
Akizungumza baada ya kutembelea watoto hao, Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka, amesema kuwa bibi huyo anadaiwa kuwafanyia watoto hao vitendo vya kikatili kwa muda mrefu na kwamba baada ya taarifa hizo kupatikana polisi walifika nyumbani kwake na kuwakuta watoto hao wakiwa katika hali mbaya na kulazimika kuwawahisha hospitalini huku bibi huyo akipelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano.
Via EATV