Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia Rehema Prosper (41), anayedaiwa kumjeruhi mpenzi wake aitwaye Timoth Samweli kwa kumwagia maji ya moto mgongoni, akimtuhumu kutoka kimapenzi na wanawake wengine.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio hilo limetokea Januari 25, 2023, katika mtaa wa Bujingwa Manispaa ya Ilemela, ambapo mwanaume huyo alienda nyumbani kwa mpenzi wake huyo Rehema ndipo tukio hilo lilipotokea.
"Sasa akapata hasira na wivu ndipo akamuua kufanya tukio hilo la kikatili kwa sasa mwanaume huyo anaendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha afya Buzuruga na hali yake inaendelea vizuri," amesema Kamanda Mutafungwa.
Katika hatua nyingine Kamanda Mutafungwa amezundua zoezi la uwekaji stika kwenye magari, pikipiki na bajaji huku akiwataka madereva kuhakikisha wanalipia fedha halali ya stika hizo.
Via: EATV