*Asisitiza wenye Leseni za Madini Mkakati kujiandaa Kimkakati
*Aeleza namna Serikali ilivyoiandaa GST kufanya tafiti za Kina
*Asema Madini ni Wizara inayotoa nafasi kubwa kushauriana na wadau
*Ataja Changamoto ya Haki Madini
Awatahadharisha wafanyabiashara wanaochukua fedha kuwaibia wageni
# Tanzania ina utajiri mkubwa wa rasilimali madini. Tuna aina zaidi ya 100 za Madini ya Vito yanayochimbwa. Tuna madini yanayotumika viwandani, madini kwa ajili ujenzi, chumvi kama chakula, tuna metali na mengine mengi.
# Nchi yetu imefunguka kwa kiasi kikubwa kiuwekezaji. Kwenye madini ya kimkakati tunafanya tafiti mbalimbali, Gesi adhimu ya Helium inafanyiwa utafiti, madini ya nikeli yanafanyiwa utafiti, jotoardhi inafanyiwa utafiti na madini mengine. Si kwamba tumeharakishwa bali inatokana na mahitaji ya dunia. Tayari tunao mkakati wa kuyatafiti kujua yako wapi kwa kiasi gani, tutajenga viwanda vyetu kuyachakata hapa, hapa nchini.
# Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ilikuwa inafanya tafiti za awali, tumebadili Sheria imepewa nguvu kufanya tafiti za kina. Tumeipa fedha kupeleka huduma za kimaabara kwa jamii, Tayari tumejenga ofisi Mkoani Geita tutajenga Chunya na maeneo mengine.
# Muda si mrefu dhahabu isiyosafishwa haitaruhusiwa kwenda nje. Taratibu za Kiserikali zitakapokamilika tutaanzisha utaratibu huo. Hivi sasa Benki Kuu ya Tanzania imeanza kununua dhahabu yetu.
# Changamoto kubwa inayoikabili Sekta ya Madini ni watu kuchanganya haki Ardhi na haki Madini. Wamiliki wa ardhi watoe haki kwa wamiliki wa haki madini kwa makubaliano.
# Wizara ya Madini ni Wizara inayofanya sana mashauriano na wadau, nia ni kusikilizana. Maboresho ya Sheria na Kanuni tuliyofanya yametokana na mashauriano na wadau.
# Wazawa kwenye Sekta ya Madini wamepewa nguvu kubwa sana. Kwenye madini ya tanzanite tumetoa fursa kwa wazawa. Leseni ndogo wamepewa wazawa.
# Mhe. Rais anaiangalia Sekta ya Madini kwa kipindi kirefu kijacho haangalii miaka 10 ijayo. Tuna bahati kimkakati nchi yetu ipo vizuri. Ipo vizuri kijiografia na miundombinu kama ujenzi wa reli ya SGR, barabara, viwanja vya ndege. Zaidi nchi yetu ina amani.
# Wafanyabiashara wasio waaminifu acheni kutumia leseni za biashara ya madini kuibia wageni. Leseni hizi zisitumike kuchafua taswira ya nchi.
# Sekta ya Madini imekua kivutio na inavutia watu wengi. Zaidi ya leseni 300 za uchimbaji wa Kati ni za wazawa na zaidi ya leseni elfu 30 ni za uchimbaji mdogo.