Godfather Mndeme (36), mkazi wa Kijiji cha Mikungani katika Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, anashikiliwa na Jeshi la Polisi akituhumiwa kumuua mkewe, Furaha Akashi (40) kisha kumfukia kisimani.
Wiki tatu zilizopita, Mndeme anadaiwa kumuua mkewe na kumfukia katika kisima hicho kisha kupanda mti na kumuajiri mtu awe anaumwagilia maji.
Akilizungumzia tukio hilo la aina yake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Justin Maseju alithibitisha kutokea na kubainisha kuwa wanawashikilia watu wawili wanaodaiwa kuhusika na tuhuma hizo za mauaji yaliyopangwa kabla na baada ya utekelezaji wake.
“Hivi sasa nipo kwenye kikao siwezi kuzungumza zaidi, ila ni kweli tukio limetokea na tunawashikilia watu wawili akiwamo mume wa marehemu wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo,” alisema Kamanda Maseju.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mikungani, Idd Salum alisema mauaji hayo yanadaiwa kutekelezwa Januari 7 na walipolibaini hilo walilazimika kuufukua mwili wa marehemu ambao ulizikwa tena jioni ya Januari 29 baada ya kukamilishwa na utaratibu wa kiuchunguzi na hatua za kisheria.
Salum alisema mtu huyo anadaiwa kumuua mkewe na kuufukia mwili wake kwenye kisima kilichokuwa kinatumika kisha akapanda mti.
Alisema wawili hao hawakubahatika kuzaa ila mwanamke alikuwa na watoto wawili aliozaa na mwanaume mwingine ambao kwa sasa wanaendelea na masomo wilayani Longido.
Alisema chanzo cha ugomvi kilichosababisha kifo hicho bado hawajakibaini ila kuna majirani walitoa taarifa kuwa Mndeme alionekana akitoa vyombo kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi na familia yake.../
Soma zaidi >>HAPA<<
Chanzo: Mwanachi