Breaking

Tuesday, 14 February 2023

NHC YAIKABIDHI SERIKALI ENEO LA UJENZI WA SPORTS ARENA



Na John Mapepele

Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo imepokea kutoka Shirika la Nyumba ( NHC) eneo la ekari 12 Kawe Jijini Dar es salaam litakalojengwa Ukumbi wa Kimataifa wa kisasa wa Michezo (Sports Arena).

Akizungumza na Wanahabari mara baada ya kukabidhiwa, Waziri wa utamaduni sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa aliyeambatana na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi amesema, Wizara inakwenda kulikabidhi eneo hilo mwezi Machi kwa Mkandarasi na ujenzi utachukua muda wa miezi 08 hadi 10 umekamilika

Aidha, Mhe. Mchengerwa ameeleza kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha sekta ya burudani na michezo zinakuwa Sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa na wananchi wananufaika nazo.

Amesisitiza kuwa watanzania wana kiu ya kuona Ukumbi wa Kimataifa wa michezo kama zilivyo nchi zingine unajengwa nchini Tanzania.

Amefafanua kuwa Kujengwa kwa ukumbi huo utabeba watu zaidi ya elfu 16 ambapo na kuwa miongoni mwa Areana kubwa Afrika ambapo kwa sasa Arena kubwa ipo nchini Senegal inayochukua watu elfu 15.

"Arena yetu itachukua watu elfu 16 na tunategemea pia ichukue watu hadi elfu 20 ili Watanzania wapate nafasi kushuhudia matamasha mengi katika ukumbi huo."

Ameongeza kuwa watanzania wamekuwa wakihoji kuwa tayari bajeti imepitishwa lakini hawaoni utekelezaji wa ujenzi wa ukumbi huo lakini amewatoe hofu kuwa sasa Serikali inakwenda kuandika historia nchini kwa kujengwa kwa ukumbi huo wa Kimataifa."

Pia ameeleza Arena hiyo inatarajiwa kukamilika kwa miezi 08 hadi 10 ambapo utakuwa ukumbi wa Kimataifa barani Afrika.

"Tulipotoka hatukuwa na mipango mizuri hivyo tulivoingia na wasaidizi wangu tumehakikisha tunaenda kuongeza nguvu kubwa tutengeneze mipango,tutengeneze michoro na hatua zote tumekwisha kuzikamilisha.

Amewahakikishi watanzani kuwa Wizara haitalala na itaendelea kukamilisha maagizo yote ya Mhe. Rais na Serikali yake katika kuimarisha sekta za Utamaduni Sanaa na Michezo ikiwa ni pamoja na kukamilisha mara moja ujenzi wa ya kimataifa hapa nchini.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages