Na John Mapelele
Katika kuimarisha utendaji wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Nchini, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe, Mohamed Mchengerwa, amemteua Addo November kutoka kwenye tasnia ya muziki nchini kuwa Mjumbe wa Bodi hiyo.
Mhe. Mchengerwa amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Ibara ya tatu (3) Kifungu cha 3.1 cha Katiba ya Mfuko huo, ambapo uteuzi huo unaanza leo na utadumu kwa miaka mitatu.
Aidha, Mhe. Waziri ametengua uteuzi wa wajumbe watatu wa Mfuko huo baada ya kukosa sifa ya uwakilishi wa makundi mahsusi ya kisekta waliyoyawakilisha wakati wa uteuzi wao kwa maslahi mapana ya Taifa,
Wajumbe hao ni Bi. Frida James Kombe, Bw. Godfrey Baltazar na Bw. Salum Mbaruku Twiza.