Breaking

Tuesday, 24 January 2023

WATUHUMIWA WAWILI WAKAMATWA NA SAMAKI KILO 980 WALIOVULIWA KWA BARUTI



Na Lango La Habari 

Jeshi la Polisi Kikosi cha Wanamaji Dar es salaam kwa kushirikiana na Wizara ya Uvuvi na Mifugo wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wawili wakiwa na samaki KG 980 zilizokuwa ndani ya boti wanasadikika kuvuliwa kwa kutumia Baruti.

Akithibitisha hilo leo Januari 24, 2023 Kamanda wa kikosi cha Wanamaji ACP Moshi Sokoro amesema kuwa Watuhumiwa hao wamekamatwa 12/01/2023 majira ya asubuhi huko maeneo ya soko la Samaki Ferry wakiwa na boti yenye usajili namba Z. 103585 jina MV MAEDRA.

Kamanda Sokoro amesema taratibu za kuwafikisha watuhumiwa mahakamani zinaendelea.

"Jeshi la Polisi linaendelea kuwashukuru na kutoa pongezi kwa wananchi wote ambao wanachukia uhalifu na linawaomba waendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wahalifu hao"

Aidha Jeshi la Polisi linaendelea kutoa onyo kwamba halitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayejihusisha na uvuvi haramu pamoja na makosa mengine ya kijinai.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages