Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi leo wamefanya kikao na ujumbe wa Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Rejine Hess na kukubaliana kushirikiana kurejesha mabaki ya miili ya machifu na vifaa vyasanaa vilivyochukuliwa wakati wa ukoloni.
Kikao hiki ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan la kuitaka Wizara kurejesha mabaki ya miili ya machifu nchini alilolitoa mjini Moshi kwenye Tamasha la Machifu Januari 21, 2022 na kikao cha machifu kilichofanyika mkoani Shinyanga.
“Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo mahususi baada ya kikao chake na Kansela wa Ujerumani ambapo katika kikao hicho iliazimiwa ufuatiliaji wa karibu kuhusu vitu vya asili vya utamaduni na mambo mbalimbali ambayo koloni la Ujerumani lilifanya wakati wa utawala wake na sisi kama Wizara tukaona kuna umuhimu mkubwa sana wa kufuatilia ili tuweze kurejesha mabaki ya miili ya machifu ” ameongeza Mhe. Mchengerwa.
Aidha, amesema tayari Serikali ilipokea maombi kutoka kwa machifu kwa ajili ya kutaka miili ya viongozi hao na tayari wizara imeshafanya tafiti ya kuona vitu vilivyopo nchini Ujerumani na kuwasiliana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na ubalozi wa Tanzania nchini.
Ameishukuru Serikali ya Ujerumani kupitia kwa Balozi wa Ujerumani hapa nchini kwa kuona umuhimu wa kuanza kiurejesha mabaki hayo ya miili na thamani za sanaa (artcraft) zilizochukuliwa kwenye maeeneo mbalimbali.
Pia amesema Serikali yaTanzania inaanza kufanya mijadala na Serikali ya Ujerumani ili kuona ni jinsi gani Ujerumani itafidia Tanzania kwa namna ilivyoathiri jamii hizo katika kipindi cha ukoloni wa ujerumani hapa kwetu.
Katika mazungumzo hayo pia Tanzania na Ujerumani zimeahihi kuimarisha ushirikiano kwenye sekta za utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katika mazungumzo hayo pia Tanzania na Ujerumani zimeahihi kuimarisha ushirikiano kwenye sekta za utamaduni, Sanaa na Michezo.