Breaking

Tuesday, 3 January 2023

MIKUTANO YA HADHARA RUKSA - RAIS DKT. SAMIA


Na lango la habari 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuondoa rasmi tangazo la zuio la kufanya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa.

Rais Dkt. Samia ametangaza hivyo leo Jumanne Januari 03, 2022 wakati akizungumza na Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa Ikulu Dar es Salaam.


"Kwa sheria zetu ni haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano yao ya hadhara...uwepo wangu leo mbele yenu ni kuja kutoa ruhusa...kwamba lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondoka" Rais Dkt. Samia
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages