Breaking

Saturday, 21 January 2023

TAKUKURU YATANGAZA NAFASI ZA AJIRA


Na Lango la Habari

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imetangaza nafasi za ajira kwa vijana wenye umri usiozidi miaka 30.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Januari 21, 2023 na takukuru imeeleza kuwa nafasi 220 za maofisa upelelezi na nafasi 100 za wapelelezi wasaidizi daraja la tatu.

Waombaji wa nafasi ya maofisa upelelezi wanatakiwa kuwa na Astashahada au shahada ya kwanza katika kozi ya uhandisi, usanifu, sayansi ya kompyuta, sheria na saikolojia.

Pia wapelelezi wasaidizi daraja la tatu, wanaohitajika ni waliohitimu elimu ya sekondari na mafunzo yoyote yanayotambulika ikiwemo ya ufundi kutoka katika taasisi zinazotambulika.

Maombi yatumwe kupitia www.pccb.go.tz/ajira

Aidha Taarifa imeeleza kuwa mwisho wa kutuma maombi ni Februari 10, 2023.







Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages