Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kansela wa Ujerumani Mhe. Olaf Scholz, Davos nchini Uswizi tarehe 18 Januari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji ambaye pia ni Mwazilishi wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) Profesa Klaus Schwab Mjini Davos nchini Uswizi tarehe 18 Januari, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Poland Mhe. Andrzej Duda mara baada ya mazungumzo Davos nchini Uswizi tarehe 18 Januari, 2023
*********************************
Rais Samia amesema Tanzania imetengeneza fursa za kitaifa kwa ajili ya mabadiliko ya mfumo wa chakula unaotarajia kuongeza uzalishaji wa chakula, kuimarisha maisha ya watu na kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Akichangia kwenye mada inayohusu masuala ya chakula ‘Food Action Partnership: Investing in Greater Resilience’, ikiwa mkutano mwingine wakati wa Jukwaa la Uchumi Duniani, Uswizi Rais Samia alizungumzia dira ya mabadiliko ya kilimo Tanzania.
Katika kudhibiti mfumo endelevu wa chakula nchini, Rais Samia amesema jitihada kadhaa zimefanyika, ikiwemo kuanzisha mradi kwa ajili ya vijana huku wakiendelea kuimarisha ukuaji wa shoroba za kilimo.
Jitihada nyingine zilizofanyika kuanzia mwaka huu wa fedha ni pamoja na kuongeza bajeti ya kilimo mara 4 ukilinganisha na ile iliyopita. Aidha, Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika mwezi Septemba kudhihirisha maendeleo hayo.
Mdahalo huo ulihudhuriwa na zaidi ya Viongozi 50 kutoka Afrika, Asia, Ulaya na Marekani kwa nia ya kuongeza kasi ya ushirikiano na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya kila nchi.
Wachangiaji wakuu katika mdahalo huo mbali na Rais Samia walikuwa Rais Gustavo Petro wa Colombia, Tran Hong Ha, Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam na Bw Alvaro Lario, Rais wa Wakfu wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Roma.