Breaking

Saturday, 14 January 2023

RC SOPHIA MJEMA ATEULIWA KUWA KATIBU ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalum cha kwanza cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa kwa Mwaka 2023 kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2023.

Kikao hicho kimemteua Sophia Edward Mjema ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Shinyanga anakuwa katibu wa Itikadi na uenezi CCM taifa akichukua nafasi na Hamdu Shaka.

Kikao hicho cha halmashauri kuu ya taifa CCM ambapo kimefanya uteuzi wa viongozi wa kamati kuu.

Miongoni mwa waliochaguliwa Tanzania bara ni Mizengo Pinda, Hassan Mwakasuvi, Halima Mamuya, Mohamed Abood Mohamed, Eng. Nassir Ally.


Via: Malunde 1 blog
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages