Breaking

Friday, 6 January 2023

RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA DIWANI, ATEUA MWINGINE




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani Msuya, aliyemteua tarehe 03 Januari, 2023 kuwa Katibu Mkuu Ikulu.

Aidha, Rais Samia amemteua Mululi Majula Mahendeka kuwa Katibu Mkuu Ikulu, Mahendeka alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.

Itakumbukwa juzi January 03,2023, Rais Samia Suluhu alimteua aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania, Kamishna Diwani Athumani Msuya kuwa Katibu Mkuu Ikulu akichukua nafasi ya Moses Kusiluka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages