Breaking

Tuesday, 24 January 2023

RAIS DKT. SAMIA ATUMBUA MKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NNE



Na Lango La Habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya utenguzi wa Mkuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri nne.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Januari 24, 2023 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Dkt. Samia ametengua uongozi wa BW. Reuben Ndiza Mfune ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali.

Rais Dkt. Samia amemtengua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma BW. Msongela Nitu Palela

Amemtengua BW. Michael Augustino Matomora aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Singida;

Amemtengua BW. Linno Pius Mwageni, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Shinyanga; na

Aidha amemtengua BW. Sunday Deogratius Ndori, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Njombe.

Taarifa imeeleza kuwa utenguzi huu ulianza tarehe 22 Januari, 2023.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages