Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Ellen Mkondya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa - Muhimbili. Dkt. Mkondya ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
(2) Amemteua
Bw. Justine Peter Mwandu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la
Bima la Taifa (NIC). Bw. Mwandu ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya
Tanzania Reinsurance (TANRE).
(3) Amemteua Prof. Verdiana Grace
Masanja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania
(TAFORI). Masanja ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson
Mandela.
(4)
Amemteua
Bw. Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha
Sheria Tanzania. Bw. Mwakapeje alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Huduma za Kisheria
kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria. Bw. Mwakapeje anachukua nafasi ya Bw.
Casmir S. Kyuki ambaye atamaliza kipindi chake tarehe 07 Januari, 2023.
(5)
Amemteua
Bi. Fatma Mohamed Abdallah kuwa Mkurugenzi
Mwendeshaji wa
Puma Energy Tanzania. Bi. Abdallah ni Meneja wa Kampuni ya Puma Energy nchini
Geneva. Aidha, Bi. Abdallah anachukua nafasi ya Dominic Dhanah ambaye amemaliza
muda wake.
(6) Amemteua
BW. David Zacharia Kafulila kuwa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na
Sekta Binafsi (PPP). BW. Kafulila ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mstaafu.
Teuzi hizi zinaanza mara moja.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu