RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua ndugu Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA).
Kupitia taarifa iliyotolewa leo Januari 16, 2023 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza Januari 10, 2023.
"Kufuatia kufutwa kwa Sheria ya Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ya mwaka 1996 na kutungwa Sheria ya Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ya mwaka 2022.
"Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua ndugu Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA),"imeeleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndugu Yusuph Juma Mwenda alikuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).