Na Thomasi Kiani, Singida
Habari za tukio hilo kupitia Gazeti la Raia Mwema zinasema Ramadhani Hamisi alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa Alli Athumani muda mrefu alishawakuta mara nyingi na alionywa na Ally aache mchezo huo na mke wake na usiku wa Ijumaa Ally aliwakuta wako naye nyumbani kwake wakati yeye alikuwa anaangalia mpira .
Kwa mujibu wa habari zilizotolewa juzi na mwenyekiti wa kijiji cha kaselya Wazzael Majja zilisema tukio hilo lilitokea saa 4:00 usiku eneo la kitongoji cha Musisi karibu na Kaselya mabandani Ikidaiwa Ramadhani alikutwa Kitongoji cha Musisi karibu na Kaselya mabandani Ikidaiwa Ramadhani alikutwa usiku huo na Mke wa Alli Athumani Nyumbani kwake.
Habari zinasema baada ya Ally kuwakuta Ramadhani akiwa na mke wake usiku huo nyumbani kwake wakaanza ugomvi na kufukuzana na kwa sababu ilikuwa kuna giza wakapotezana njiani, Ally akamvizia nyumbani kwao na muda si mrefu Ramadhani alifika nyumbani kwao hajui kuwa aliviziwa na Ally
Habari zinaeleza Ramadhani hakujua kuwa Alli alijificha mahali akimvizia akiwa hajui kinachoendelea ghafla alijitokeza alikojificha akamrukia akamkamata akamzidi nguvu akamchoma tumboni na kitu kikali chenye ncha kali akamchoma upande wa kulia Damu zikamtoka na utumbo ukajitokeza nje akaanguka chini
Ali baada ya kuona mgoni wake kaanguka chini baada ya kumchoma kisu alienda moja kwa moja kwa mzazi wake Ramadhani Ally Mzee Hamisi akapiga hodi alipoitikiwa akamwambia mzee Hamisi atoke nje akamuone mwanae anakufa”Mimi tayari kazi nimeimaliza nimemkuta mwanao anamchezea mke wangu” akaondoka.
Imeelezwa mzee Hamisi alipotoka nje akamkuta mwanae akiwa hajiwezi damu zinamtoka tumboni nguo zake zimemchafuka na utumbo unajitokeza nje kwanza akachanganyikiwa , lakini Ramadhani akiwa bado anafahamu kidogo akamwambia baba yake, nikifa nimeuwawa na Ali amenichoma na kisu akakimbia.
Mzee Hamisi baada ya kumkuta mwanae akiwa katika hali ile akapiga yowe majirani walifika na waowakapiga filimbi watu wakafika wengi kwenye tukio hilo mara moja wakaamua Ali na mke wake wakamatwe wawekwe chini ya ya ulinzi na Ramadhani apelekwe Hospitali ya mkoa Singida kwa uangalizi na matibabu.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Msisi Haruna Hamisi amesema, majeruhi alipelekwa usiku huohuo Hospitali ya Singida kwa gari baada ya wanaichi kumsaidia huduma za kwanza kwa kumfunga nguo jeraha hilo lakini waganga wa Hospitali hiyo walijitahidi kuokoa maisha yake lakini haikuwezekana muda mfupi baadae akafariki dunia kwa kutokwa na damu nyingi na jeraha lilikaa pabaya
Afisa mtendaji wa kata ya Kaselya Rehema Fanuel alipotakiwa na mwandishi wa habari hizo atoe maelezo aliyonayo juu ya tukio hilo juu ya mwenyekiti wake wa vijana wa kata yake kuuwawa alikataa kutoa maelezo lakini Mwenyekiti Haruna Hamisi amesema watu waliotumwa kumthibiti Ally na Mke wake hawakuwakuta, wote walishaondoka usiku uleule na hawajulikani walikokwenda hadi sasa.
Polisi wa kituo cha Ndogo walifika kwenye tukio hilo jumamosi wakakuta wahusika wa tukio hilo Ally na Mke hawapo walishakimbia usiku hivyo wamewataka wananchi wa kata ya Kaselya kushirikiana na jeshi hilo kuwasaka watuhumiwa wafikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu mashtaka yao.
Polisi Iramba imewataka wananchi wa kata ya Kaselya na Iramba yote kushirikiana na polisi ili watu hao wakamatwe hata kama wameikimbia kata yao hata kile walikokimbia wafuatiliwe na vyombo vya dola na wananchi hakuna mtu aliyeruhusiwa kuuwa mwenzake hiyo ni kuvunja sheria na katiba ya nchi ni lazima wakamatwe.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida hakuweza kupatikana kwa simu yake kuelezea ripoti alizopata kutoka Iramba kuhusiana na tukio hili la Mwenyekiti UVCCM kata ya Kaselya Kufa kwa kuchomwa Kisu
Mwisho