Breaking

Wednesday, 4 January 2023

MWANAJESHI WA UGANDA AWAGEUKA WENZAKE WATATU NA KUWAUA KWA RISASI SOMALIA



Mwanajeshi wa Uganda chini ya Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (Atmis), anadaiwa kuwapiga risasi wenzake watatu na kuwaua jijini Mogadishu Jumatatu, Januari 2, asubuhi.

Kwa mujibu wa ripoti ya BBC, tukio hilo la ufyatuaji risasi lilitokea katika makao makuu ya kikosi cha jeshi la Uganda.

Msemaji waJeshi la Uganda, Felix Kulaigye, alithibitisha kisa hicho na kusema mwanajeshi huyo alikamatwa.

Inaripotiwa kuwa mwanajeshi huyo alimvamia na kumpiga risasi mwathiriwa wake wa kwanza kifuani.


Huku wanajeshi wakidhani kuwa kambi yao ilikuwa imeshambuliwa, mwathiriwa wa pili alipigwa risasi tatu kichwani alipokuwa akijaribu kujua kinachoendelea.

Kisha mwanajeshi wa tatu alipigwa risasi mgongoni alipokuwa akijaribu kutoroka.

Milio hiyo ya risasi ilikoma baada ya afisa mwingine alipofaulu kumkamata mtuhumiwana kumpokonya silaha.

Inakumbukwa kuwa tukio sawia na hilo liliwahi kutokea mwaka wa 2019, wakati nahodha wa Uganda alijiua baada ya kumpiga risasi mwenzake na kumuua.




Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages