Omar Bin Laden mwanawe mwasisi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda, Osama bin Laden, amefichua taarifa za kushangaza kumhusu baba yake.
Akizungumza katika mahojiano na gazeti la The Sun, Omar Bin Laden alikiri kwamba kuna baadhi ya mambo ambayo baba yake alifanya yaliyomkera zaidi.
Miongoni mwa mambo ambayo alifichua hayakumfurahisha ni kwamba baba yake alifuga mbwa ambao kulingana na dini ya Kiislamu huchukuliwa kama uchafu.
Omar Bin Laden alisema kuwa babake Osama Bin Laden alifanyia majaribio mbwa wake silaha za kemikali.
"Niliona (vipimo vya silaha za kemikali vikifanyiwa mbwa, sikufurahia jambo hilo. Nilijaribu kusahau kumbukumbu hizo zote mbaya kuhusu tukio hilo. Ni vigumu lakini baada ya muda, utasahau," alisema Omar Bin Laden.
Kitabu kilichoandikwa kuhusu Osama Bin Laden kinasema kwamba mbwa huyo alikufa ghafla lakini hakuna anayejua kwa nini alikufa.
Osama bin Laden aliuawa katika operesheni iliofanywa na wanajeshi wa Marekani mjini Abbottabad, Pakistan na mwili wake ulirushwa katika Ziwa la Arabian kutoka kwenye ndege ya Amerika saa kadhaa baada ya kifo chake, ili kuzuia kuundwa kwa kituo cha hija ardhini.
Hata hivyo, Omar bin Laden ambaye sasa ana umri wa miaka 41, anasema haamini kuwa Marekani ilizika mwili wa babake Osama bin Laden baharini.
Omar aliishi nchini Sudan na baba yake Osama Bin Laden kuanzia mwaka 1991 hadi 1996 kabla yao kutengana akikiri kwamba alipata mafunzo ya matumizi ya silaha katika kambi za mafunzo za al-Qaeda.
Katika kilichoandikwa kuhusu Osama Bin Laden, Omar alisema haikubaliki kwa baba yake kuua raia, na ndiyo maana aliondoka Al-Qaeda.
Hata hivyo, baba yake hakufurahishwa na uamuzi wake alirejea Saudi Arabia na kuanza biashara mwaka 2006 na baadaye alikwenda Ulaya.