Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 6 amempiga risasi na kumjeruhi mwalimu wake, katika jimbo la Virginia.
Mwanafunzi huyo mvulana, amekamatwa na polisi baada ya tukio hilo katika shule ya msingi ya Richneck.
Mkuu wa polisi Steve Drew amesema kwamba tukio hilo halikuwa la kimakosa na kwamba mwalimu, mwanamke mwenye umri wa miaka 30, amepata majeraha mabaya yanayotishia uhai wake.
Hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Hakuna taarifa kamili kuhusu namna mtoto huyo alivyoapata bunduki.
Shughuli za masomo katika shule tukio lilitokea, zimesitishwa na hakuna masomo yataendelea Jumatatu.
Via: Global Publisher