Breaking

Friday, 20 January 2023

MTOTO AKUTWA AKINYONYA TITI LA MAMA YAKE ALIYEUAWA



Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja amekutwa usiku akiendelea kunyonya ziwa la mama yake ambaye anadaiwa kuuawa na mumewe, Jeshi la Polisi mkoani Manyara limethibitisha.

Katika uhalifu huo dhidi ya mama huyo, Sabina Barma (28) ambaye maiti yake ilikutwa imefungwa mikono, inadaiwa kifo chake kimetokana na kudhuriwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni akiwa nyumbani kwake.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Gisigisi, Kijiji cha Saydoda, Kata ya Ufana wilayani Babati, John Manonga, alisema walimkuta mtoto akinyonya ziwa la mama yake, bila ya kujua kuwa ameshafariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, George Katabazi, alithibitisha mwanamke huyo aliuawa juzi majira ya saa tatu usiku.


Chanzo: Nipashe
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages