Breaking

Thursday, 12 January 2023

KISHAPU YAADHIMISHA MIAKA 59 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA KUPANDA MITI 1000



Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude ameongoza zoezi la kupanda miti 1000 ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Zoezi hilo limefanyika leo Alhamisi Januari 12, 2023 pembezoni mwa eneo la Bwawa la maji kijiji cha Kishapu likiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude ameambatana na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwepo katibu Tawala wa Wilaya, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali Wilayani Kishapu.

Akizungumza baada ya zoezi hilo DC Mkude aliwashukuru waliojitokeza katika zoezi hilo na kutoa wito kwa wananchi kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda miti ikiwemo ya matunda.

"tuzitumie vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kupanda miti hasusani miti ya matunda lakini pia miti hii inayotunza maji tutaendelea kupata katika Vyanzo vyote vya maji"



DC Mkude ameeleza kuwa jitihada kubwa za Serikali ambazo zinafanywa kulinda mazingira ziungwe mkono na wananchi kwani ni jukumu la kila mmoja.

Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka Wananchi wote wanaozamia katika eneo hilo kwaajili ya kufanya kilimo na makazi kupisha mala moja kuepusha uchafuzi wa mazingira.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Ndugu Emmanuel Johnson, amesema kuwa maeneo ya Wilaya ya Kishapu yana mvua kidogo hivyo wanategemea sana kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia mabwawa.



Mh. Johnson Amesema serikali imetenga fedha kwa ajili ya kufufua mabwaya yaliyoharibika ili yaweze kusaidia wakulima na wafugaji.

" jitihada ambazo zinafanyika kwa sasa ni kufufua mabwawa yaliyoharibika, tumefufua Bwawa la Kiloleli, Mihama na Beledi, Kwa Mwaka huu Halmashauri imetenga Fedha kwaajili ya kufufua mabwawa zaidi kauli mbiu yetu ni kuhakikisha Wilaya yetu inakuwa na mabwawa zaidi kwaajili ya kilimo na ufugaji".

Naye Diwani wa kata ya Kishapu Joel Charles Ndettoson ameeleza kuwa Bwawa hili linahudumia zaidi ya kata Nane na Wilaya jirani ya Maswa Mkoani Simiyu.

"Bwawa hili linasaidia zaidi ya kata nane, Bwawa hili mbali na wanakijiji wanaotumia Kuna Shughuli za kimaendeleo zinazotumika eneo hili tumeona leo tupande miti zaidi ya 1000 pia tumeweka mikakati ya kusimamia Bwana hili ili liendelee kutusaidia.



Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kishapu Bw Elikana Masanja amefurahishwa na ujio wa Mkuu wa Wilaya pamoja na msafara wake kwa uamzi wa kupanda miti katika eneo hilo

"Nafurahia sana kwa ujio wa Mkuu wa Wilaya katika Bwawa hili na kuamua kupanda miti katika eneo hilo kwa Sababu itasaidia sana katika utunzaji wa Vyanzo vya maji na Bwawa hili litareje katika thamani yake.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages